Na Kareny
Masasy, Kishapu
MWAMKO mdogo wa elimu kwa wazazi wa
kata ya Bunambiyu halmashauri ya
wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imebainika
kuwarudisha nyumba maendeleo ya watoto wao kielimu kwa kuthamini kuwatumikisha kazi za shambani na kuchunga mifugo.
Licha ya
hali hiyo pia wamekuwa wakiwaeleza wanafunzi wa kike wafanye vibaya katika mitihani yao ya
kumaliza elimu ya msingi ili wasifaulu
na baadaye waolewe lengo la mzazi kupata utajiri wa ng’ombe.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ng’wang’hili iliyopo kijiji hicho Emmanuel
Magesa anasema kuwa kumekuwepo na
mdodoko wa wanafunzi kushindwa kumaliza
shule kwasababu yakupewa majukumu ya
kuchunga mifugo.
Hata hivyo
anasema kuwa hali hiyo inasababishwa
na baadhi ya wazazi kuwa na mwamko mdogo
wa elimu ambapo changamoto nyingine
wamekuwa wakihamisha watoto wao bila kutoa taarifa yoyote.
“Anasema
mfano waliopo darasa la saba sasa hivi
walianza darasa la kwanza mwaka 2012
wakiwa 51 ambapo wavulana ni 22 na wasichana ni 29 na
hadi leo hii kuna wanafunzi 19 tu
ambao wanatarajia kufanya mtihani wasichana 8 na wavulana 11”anasema mwalimu mkuu wa shule hiyo..
Mwalimu
Magesa anasema kuwa mafanikio ya elimu
bure yamefanya uandikishaji wa wanafunzi
wa darasa la kwanza kutoka wanafunzi
50 kwa miaka ya nyuma hadi
kufikia wanafunzi 112 kwa sasa.
Pia uandikishaji
wa darasa la awali ulikuwa
wanafunzi 25 zamani hadi kufikia 100 ambapo idadi inaanza
kupungua taratibu pindi wanapoanza
kuingia darasa la tano hadi la saba
sababu wameonekana kukua kwa kutumikishwa kazi za shambani na kuchunga mifugo.
Magesa
anasema kumekuwepo na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaeleza watoto wao wafanye
vibaya siku ya mtihani wakumaliza elimu
ya msingi katika hali ya matokeo kuanzia mwaka 2015 shule hiyo walimaliza wanafunzi 22 na wawili tu ndio waliofaulu kuendelea na
elimu ya masomo ya sekondari.
Pia mwaka
2016 wanafunzi waliofanya mtihani darasa la saba walikuwa 21
ambapo wavulana ni tisa na wasichana 12
na wote walifaulu ikiwa mwaka 2017 waliofanya mtihani ni 19 na nane
hawakufaulu ambao wavulana ni watatu na wasichana ni watano.
Anasema licha yakuwepo utoro wa rejareja
unaosababishwa na miundombinu mibovu hasa kipindi cha masika ambapo darasa la
awali na darasa la kwanza hawaji shule
na hata ukimrudisha mwanafunzi amfuate mzazi wake aje mzungumze ndio
umempatia unafuu wa mwanafunzi kuendelea
kukaa nyumbani na mzazi haji.
![]() |
Mwanafunzi wa shule ya msingi Ng'wang'hili kata
ya Bunambiyu aliyeacha shule akiwa darasa la tano nakuendelea
kuchunga mifugo ya wazazi wake. Picha na Kareny Masasy.
|
Baadhi ya
wazazi wa kata ya Bunambiyu Modesta
Obedi na Ernest Hausa wanasema kuwa wazazi wamekuwa wakishikwa na tamaa ya
kupata utajiri wa ng’ombe kwani wamekuwa wakiwaeleza wanafunzi wa kike kufanya
vibaya katika mitihani yao ya mwisho ili waweze kuolewa na mzazi kumiliki
ng’ombe jambo ambalo anaona ni ufahari kwake.
Ernest Hausa
anasema kuwa kweli wapo wazazi
wanaowatumikisha wanafunzi kazi za shambani msimu wa kilimo anaona wanao uwezo
wa kulima msimu wa mvua umefika hakuna nguvu kazi bora aende akamuombee ruhusa
shuleni kwa kusema uongo
nakumtumikisha kuliko apate
elimu.
Licha ya
suala la uchungaji mifugo pia anasema
huwatumikisha shambani kwaajili yakulima vibarua kwenye shamba la mtu nakupata fedha za chakula msimu wa mvua za masika kipindi cha kilimo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ngw’ang’hi
Buzali Mabele anasema kuwa wazazi wamekuwa wakiwaachisha shule watoto wao
ili kuchunga mifugo na kulima au kuhama bila kutoa taarifa na kuwaozesha umri
mdogo hilo sasa limeingizwa kwenye
mpango mkakati wa kijiji kuzibiti hali hiyo
isiendelee kwa kuwachukulia hatua za kisheria.
Mtendaji wa
kijiji cha hicho Thomas Nyonyo
anasema kuwa hivi sasa wameanza kuzibiti utoro kwa kuwasaka wazazi ambao wanahama kimya
kimya na watoto wao ambao wanasoma
shule na kuwaeleza kuacha tabia ya
kuwarubuni wafanye vibaya kwenye mitihani yao yakumaliza elimu ya msingi.
Wengine
wazazi wamekuwa wakiwatumikisha shughuli za
shambani na kuchunga mifugo kwa kuona kwenda shule ni kero kubwa kwani
idadi kubwa ya wazazi hawajasoma isitoshe ni jamii ya wafugaji hasa
wanaoishi katika kijiji utakuta
mwenye ng’ombe chache ni 50.
Diwani wa
kata ya Bunambiyu Richard Sangisangi
anasema kuwa kweli wazazi bado wanamwamko mdogo wa elimu wamekuwa wakiwaachisha watoto wao kwenda shule ili
wafanye kazi za shambani au kuchunga mifugo hilo limepigwa marufuku
atakaye bainika mzazi atachukuliwa hatua na miundomibu ya
barabara msimu wa mvua unachangia utoro
wa rejareja kwa wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba
anasema kuwa suala la wazazi wafugaji
kutoruhusu watoto wao kwenda shule hilo
lipo ila walikuwa wakielezwa umuhimu wa elimu na kuwachukulia hatua wazazi
watakao bainika kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo
Talaba anasema kuwa tayari yamekwisha tolewa maagizo kwa
watendaji wa vijiji na kata kufuatilia wanafunzi watakao watoro wanaosababishwa na kutumikishwa kazi
mashambani na kuchunga mifugo ili wazazi waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Kweli jamii
ya wafugaji watoto wao wamekuwa hawasomi na wilaya hii asilimia 88 ni wafugaji
na wakulima ndio wanategemea kwa
kuwainulia kipato lakini tabia ya kutowaombea
uhamisho shuleni ipo, hata
ukitaka kuwachukulia hatua wazazi unashindwa
utawapatia wapi?”alisema mkuu wa
wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Kishapu Stephen
Magoiga anasema kuwa baadhi ya wazazi
wamekuwa wakienda shuleni kuwaombea ruhusa watoto wao wanaumwa kumbe ni uongo
wamekuwa wakifanya hivyo lengo kuwapeleka shambani kulima au kulichunga mifugo.
“Kuna mzazi
mmoja tulielezwa amemuombea ruhusa mwanaye kuwa anaumwa lakini tulifuatilia
mpaka shambani alipoenda yeye na mwanaye tukamkuta shambani mzazi huyo
alichukuliwa hatua lakini aliomba msamaha kuwa
hatorudia tena tena ambapo ndio imekuwa tabia ya baadi yao wazazi”alisema mkurugenzi.
Hata hivyo
mkurugenzi Magoiga anasema kuwa kuna shule
za msingi 117 ambazo baadhi
yao maeneo yalipo wanafunzi kweli wanalazimika kutembea umbali
mrefu hasa kijiji ch Ng’wang’hili vitongoji vyake viko mbalimbali kwani
wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita zaidi ya saba kwenda shule nalo linasababisha
utoro au kuacha shule.
Anasema halmashauri hiyo matokeo ya darasa la saba
kwa mwaka jana walishika nafasi ya mwisho kimkoa katika halmshauri sita zilizopo hivyo ni
jitihada zinahitajika baada ya kuweka mkakati kwa mwaka huu kwa mwalimu mkuu ambaye shule yake ikifelisha idadi kubwa ataondolewa kwenye nafasi hiyo.
Katiba ya
Jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 inaeleza kuwa mtoto anahaki ya kulindwa na kupendwa ,anayo haki ya kupata elimu,kucheza na kujieleza pia serikali imekomesha utumikishwaji wa
watoto mashambani wala katika biashara ndogondogo
No comments:
Post a Comment