BISHAGAZI:
KISA MAFUNZO CHA HARAKATI NGAZI YA JAMII
Utangulizi:
Selemani Bishagazi ana umri wa
miaka 39, anaishi Mtaa wa Kipunguni, kata ya Kipunguni, wilaya ya Ilala, mkoa
wa Dar es Salaam. Mwaka 2011 alianza kujishughulisha na harakati za haki za binadamu
bila ya yeye mwenyewe kujua kama anachokifanya ni harakati hizo.
Anajishughulisha na biashara ya kuuza nguo za kike za mitumba maeneo ya Ubungo
External (Mabibo Hostel) kama sehemu ya kujipatia kipato cha kuendesha maisha
yake ya kila siku. Bishagazi ana mke na watoto.
![]() |
Msaada wa cherehani |
“Sherehe za kuwapongeza watoto
wa kike baada ya kufanyiwa ukeketaji zilikuwa zikifanyika hadharani kwenye
maeneo ninayoishi ya Kipunguni, walikuwa wakieleza wazi kabisa dhumuni la
sherehe hizi. Jambo hili nilipokuwa nikilishuhudia, ndipo nilipoanza kuona
kwamba haliko sawa” anaeleza Bishagazi.
Nilianza kulishughulikia sula
hili kwa kwenda kuwaona viongozi wa serikali ya mtaa, mheshimiwa diwani na hata
polisi, lakini kote huko sikupata ushirikiano wowote. Kwa mfano Mh. Diwani
aliwahi kunitamkia wazi kwamba yeye hataweza kulifuatilia jambo hili kwani
wananchi wake watamnyima kura kwenye uchaguzi utakaofuata. Kwa upande wa jeshi
la polisi ili uweze kuwatoa kituoni waende kwenye tukio ni lazima ulipe hela ya
mafuta ya gari litakalowabeba kwenda huko; au umlipe posho askari utakayepewa
kufuatana naye kwenda kwenye tukio. Haya yote yalikuwa ni changamoto kwangu.
Lakini pia kulikuwa na maneno ya kukatishwa tamaa kutoka kwa watu mbali mbali
na wengine wakidiriki hata kuniambia “anayekeketwa siyo mwanao wala nduguyo,
kinakuuma nini?” Lakini yote haya hayakunikatisha tamaa.
Bishagazi alianza kushiriki
semina za jiansia na maendeleo maarufu kama GDSS Mwezi Septemba mwaka 2013,
kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.Alifahamu semina hizo kupitia mteja wake
katika biashara zake. Katika maongezi ya
kawaida nilimdokeza kuhusu tatizo la ukeketaji kwenye maeneo anayoishi ya Kipunguni. Hapo alishauriwa kuhudhuria
semina za kila jumatano (GDSS) zinazofanyika TGNP Mtandao.Mteja huyo
akasisitiza kwamba akihudhuria semina hizi atapata uelewa zaidi, lakini pia
huenda aikapata msaada wa namna ya kutatua tatizo la ukeketaji Kipunguni na
namna ya kuendesha harakati zaidi.
Semina hizo zimesaidia sana
kuinua kiwango chake cha uelewa wa masuala mbambali, kujitambua,kujia thamani
yake kama binadamu na raia wa Tanzania,haki
na thamani ya wasichana na wanawake.kikubwa zaidi amegundua kwamba harakati
zozote zile kuleta mabadiliko huwezi kuzifanya peke yako, lazima ujenge nguvu
za pamoja.
Akiwa kama kiongozi wa kikundi cha
sauti ya wananchi Kipunguni,wameweza
kuokoa wasichana kadhaa lakini mmojawapo ni msichana Anna Nicolaus wa Kipunguni
Gongo la Mboto jijini alishawishiwa na wazazi wake ili akubali kukeketwa kwa
madai ya kuwa watampatia cherehani.Yeye alikimbia nyumabani na kukimbialia kwa
Bishagazi ambaye alimpokea na
kushirikisha wanaharakati wengine ili waone ni kwa jinsia gani
watamsaidia.Waliamua kwenda kwa mzazi ambaye ni mama na kumwelimisha madhara ya
ukeketaji ndipo akatengua maamuzi yake ya kumkeketa binti yake.
Baada ya kipindi cha miaka
miwili kikundi cha sauti ya wananchi kipunguni kilipata ugeni kutoka TGNP
Mtandao,kati ya mamabo waliyovutiwa nayo ni kisa cha bi Anna na wakaahidi
kuchanga fedha lili kumpataia Anna Charahani.Hatimaye ndoto ya Anna ikatimia kwani
tarehe 15 mwezi wa sita aliweza kukabidhiwa na diwani wa kata hiyo Mh Mohamed
Msophe charahani yake ambayo itampa ajira
kuendesha maisha yake na kujikwamua kiuchumi.Kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo akikwemo diwani wa kata ya Kipunguni
Mafanikio
ndani ya Jamii ya Kipunguni:
· Mradi wa Maji Kata ya Kipunguni
Sauti ya
Jamii Kipunguni ina wanachama zaidi ya 60 kutoka mitaa mine ya Kata ya
Kipunguni;kwa kushirikiana na wanajamii wameweza kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.Kutokana na
uhaba wa maji wanawake na watoto
walitembea umbali mrefu ,watoto kubakwa,
kinamama kupata vipigo kutoka kwa waume zao na
mmoja wa wasichana aliyekwenda kuchota maji Mto Mzinga, na huko akachukuliwa
kwa lazima na kwenda kukeketwa.
Mchakato ulianza kwa kukusanya taarifa hizo na
nyingine zilizokuwepo na kuzipeleka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry
Silaa ambaye alileta mradi mkubwa wa maji kwenye Kata ya Kipunguni wenye
thamani wa Shs. 890m/=. Ushawishi huu ulifanyika mwaka 2014, na hivi sasa mradi
uko kwenye hatua za mwisho kukamilika. Mradi huu utasambaza maji sehemu kubwa
ndani ya Kata yetu ya Kipunguni.
· Kilimo cha Mboga Mboga kwa Kinamama
Kwa ushawishi wa Bishagazi ameweza kuwaunganisha
wanawake 24 (mmoja wao akiwa ngariba) wakaanzisha kilimo cha mboga mboga, na
kilimo hiki kwa sasa kinawasaidia kupata mboga majumbani mwao, lakini pia
wanauza mboga ya ziada na kujipatia kipato. Alianza kwa kuwakodisha eneo lenye
ukubwa wa ekari 3 kwa Shs. 150,000/= ambalo sehemu ya eneo hili linatumika kwa
kilimo hiki. Kwa sasawanawake hawa wanakodisha eneo hilo kwa gharama zao. Eneo
hili liko bondeni na kuna chem chem ya maji inayotumika kumwagilia mboga.
Lakini pia kutokana na ufugaji wa kuku katika maeneo ya jirani wanaweza kupata
mbolea kwa ajili ya kilimo chao cha
mboga.
Sauti ya Jamii Kipunguni hukitumia kupenyeza agenda
mbalimbali ikiwemo ya kupambana na ukeketaji. Wamekuwa wakizungumza nao ana kwa
ana kuhusu ukeketaji na madhara yake, na umuhimu wa kuachana na mila hii
potofu. Lakini pia wakipata machapisho mbalimbali kutoka TGNP na taasisi
zinginezo.
· Upotevu wa Ushuru wa Serikali Machinjio ya
Mazizini
Sauti ya
Jamii Kipunguni ilipata taarifa kuhusu ufisadi unaofanyika kwenye machinjio ya
Mazizini yaliyoko kata ya Kipunguni. Ushuru unaolipwa kwa ajili ya kuchinja
ng’ombe machinjioni hapo kiasi kikubwa kinaishia kwenye mifuko ya wajanja
wachache ambao ni viongozi wa machinjio hayo, badala ya kwenda serikali kama
inavyotakiwa. Kwa mfano kila ng’ombe anayechinjwa Mazizini hulipiwa Shs.
10,000/=; lakini hakuna risiti yoyote ya serikali inayotolewa kwa mlipaji Mh.
Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushtukiza kwenye machinjio ya Vingunguti na
kujionea mwenyewe ufisadi mkubwa uliokuwa ukifanyika hapo. Waziri Mwigulu
alitoa maelekezo kwamba mara moja machinjio zote zitumie mashine za
kielektroniki (EFD) kutoza ushuru wa machinjio ili kuepusha upotevu wa mapato machinjioni.
Suala hili halikuishia hapo kwani niliweza pia kulipeleka na kulizungumzia
kwenye vyombo vya habari kama ITV, Radio One, East Africa Radio na gazeti la
Nipashe.
· Kujengea Uwezo Wananchi na Kuwajibisha
Viongozi:
Kwa wastani sauti ya jamii Kipunguni imeweza kuwafikia watu 1,500 na kuwajengea uwezo wa masuala mbali mbali na kwa
kiwango tofauti tofauti ndani nan je ya Kata ya Kipunguni. Hawa ni pamoja na
wananchi wa kawaida, viongozi wa kisiasa, viongozi wa serikali, watumishi wa
umma (walimu, polisi), viongozi wa vikundi na taasisi za kijamii, wazee,
wanawake, watoto wa kike, wapiga kura n.k.Pia wameweza kuwasainisha mikataba ya
makubaliano ya madai ya wanachi/wapiga kura na baadhi ya wagombea wa nafasi za
uongozi ili pindi watakapopata nafasi hizi za uongoi watekeleze yale
waliyokuabaliana na kutia sahihi zao kabla
wanachi hawajawapigia kura.
No comments:
Post a Comment